• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 1-February 7)

  (GMT+08:00) 2020-02-07 20:11:32

  FIFA yamfungia maisha nyota wa Uganda, wengine watatu wapigwa miaka kwa upangaji matokeo

  Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, limemfungia maisha kujihusisha na soka, mchezaji wa Uganda, George Mandela kutokana na upangaji matokeo.

  Mandela amefungiwa maisha huku wachezaji wengine watatu wakifungiwa miaka miaka minne kila mmoja.

  FIFA imesema kuwa Mandela, kutoka nchini Uganda alikuwa kinara wa tukio hilo la upangaji matokeo mechi za msimu uliyopita.

  Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa, Mandela alikuwa ndiyo kiungo akipokea maagizo kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya kikosi cha Kakamega Homeboyz na kumfikishia aliyekuwa kocha wake ambaye pia alikuwa raia wa Uganda. Hata hivyo klabu ilikuja kuachana na Mandela mwezi uliyopita.

  Wachezaji watatu ambao walikuwa na Mandela, ambao ni Moses Chikati, Festus Okiring na Festo Omukoto wamepata adhabu ya kifungo cha miaka minne.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako