• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 22-February 28)

    (GMT+08:00) 2020-02-28 20:29:41

    Raia wa Italia nchini Nigeria athibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

    Nigeria imethibitisha mtu mmoja nchini humo ameambukizwa virusi vya Corona. Mgonjwa huyo, raia wa Italia anayefanya kazi nchini Nigeria alisafiri kwa ndege kwenda mji wa kibiashara wa Lagos akitokea Milan tarehe 25 mwezi Februari.

    Hata hivyo Nigeria imesema anaendelea vizuri na hakuna dalili ya hatari na hivi sasa anapatiwa matibabu hospitalini Lagos.

    Nigeria imesema ilijiandaa na kuwa imekuwa ikiandaa vituo kwa ajili ya operesheni za dharura, ili kuchukua hatua za udhibiti.

    Mamlaka zimesema zimeanza kuwatambua wale wote waliokaribiana naye tangu aliporejea Nigeria.

    Zaidi ya watu 80,000 wameripotiwa kuathirika katika nchi 40. Zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha nje ya China, tangu mlipuko ulipoanza. Idadi ya maambukizi nchini China imeendelea kushuka kufuatia juhudi kubwa zinazofanywa na nchi hiyo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako