• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 22-February 28)

    (GMT+08:00) 2020-02-28 20:29:41

    Ethiopia yakabiliwa na wakati mgumu wa kupambana na Nzige wa jangwani

    Umoja wa Mataifa umeonya kuwa serikali ya Ethiopia inashindana na wakati kudhibiti uvamizi wa nzige wa jangwani unaoendelea, wakati msimu wa mavuno wa kuanzia Februari hadi Mei ukianza.

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetoa onyo hilo jipya, wakati linaiunga mkono wizara ya kilimo ya Ethiopia kupanua operesheni za anga na ardhini kwenye maeneo ya uzalishaji wa nafaka, hasa katika majimbo ya Oromia na maeneo ya kusini.

    Mjumbe wa FAO nchini Ethiopia Bibi Fatouma Seid amesema, hiki ni kipindi muhimu cha kuokoa mavuno ya hivi sasa na ya kipindi kijacho, ili kuhakikisha usalama wa maisha ya watu.

    Shirika hilo pia imetoa taarifa ikisema, kutokana na kusambaa kwa kasi kwa nzige, kuna haja ya kuongeza uwezo wa kukabiliana na uvamizi wa nzige.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako