• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 7-Machi 13)

  (GMT+08:00) 2020-03-13 19:58:50

  Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta na mchezaji wa Chelsea wakutwa na Virusi vya Corona

  Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona na mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikiendi imeahirishwa.

  The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi waklabu hiyo ambao waligusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.

  Ligi ya Premier itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.

  Arsenal inatarajia kwamba idadi kubwa ya wafanyakazi na kikosi chote cha kwanza kitalazimika kujiweka karantini.

  Klabu hiyo ilikuwa ikitarajiwa kukabiliana na Brighton katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi mwendo wa saa 11 jioni lakini Brighton ikatoa taarifa muda mfupi baada ya Arteta kugunduliwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ikitangaza kwamba mechi hiyo imeahirishwa.

  Mechi ya ligi ya Uingereza kati ya Arsenal na Manchster City pia imeahirishwa siku ya Jumatano kama hatua ya tahadhari kabla ya wachezaji kadhaa wa Arsenal kujiweka katika karantini.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako