• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 7-Machi 13)

    (GMT+08:00) 2020-03-13 19:58:50

    Kisa cha kwanza cha virusi vya corona chathibitishwa Kenya

    Kisa cha kwanza cha virusi vya corona cha thibitishwa Kenya. Wizara ya afya imethibitisha kisa hicho kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe.

    Akiizungumza na vyombo vya habari waziri huyo amesema kwamba kisa hicho kilithibitisha Alhamisi usiku.

    Waziri huyo amesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China.

    Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasili nchini kutoka Marekani kupitia mjini London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.

    Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya.

    Hata hivyo waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.

    Waziri huyo amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuwacha wasiwasi.

    Amesema kwamba serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha kwamba hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.

    Kamati ya dharura ilioanzishwa ili kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona itaendelea kutoa muongozo ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako