• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 21-Machi 27)

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:11:42

    Afrika Kusini yaongoza kwa idadi ya wagonjwa wa Corona

    Afrika kusini siku ya jumamosi ilitangaza vifo viwili vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona wakati nchi hiyo ikianza kutelekeza marufu ya kutoka nje wakati idadi ya maambukizi ikisemekana kuwa zaidi ya 1,000.

    Ijumaa, jeshi la ulinzi na usalama la Afrika kusini lilianza kuhimiza utekelezwaji wa marufuku ya kutoka nje ikiwa ni hatua ya kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Mapema kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo foleni ndefu ya watu ilionekana kwenye maduka makubwa wakifanya manunuzi muhimu ili kujiwekea akiba wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.

    Afrika kusuni imeripoti kuwa na wagonjwa zaidi ya 1,000 ikiwa ni idadi kubwa zaidi barani Afrika.

    Jioni siku ya Alhamisi rais Cyril Ramaphosa alitembelea kambi ya jeshi kabla askari hao kuruhusiwa kuingia barabarani.

    Wakati huo huo Kenya imetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Corona siku ya alhamisi.Mgonjwa huyo ambaye ni raia wa Kenya alikuwa ametokea Afrika Kusini. Hadi kufikia alhamisi idadi ya maambukizi ilikuwa imeongezeka na kufikia 31.Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya tayari ametoa maagizo ambayo yanatakiwa kufuatwa na wakenya ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe amemtaka kila mkenya kufuatwa maagizo yanayotolewa na serikali ikiwemo kufungwa kwa baa, kuzuia mikusanyiko na mikutano ya hadhara.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako