• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 21-Machi 27)

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:11:42

    Marekani yaongoza duniani kwa visa vya maambukizi ya corona

    Marekani imedaiwa kuwa nchi yenye idadi kubwa ya visa vya maambukizi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani. Hivi sasa inadaiwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

    Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeishinda China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

    Nchini Marekani vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 vimethibitishwa, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

    Idadi kubwa ya maambuizi imekuja wakati ambapo rais Donald Trump anategemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu. Rais Trump alieleza namna alivyosikitishwa na idadi ya maambukizi.

    Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona virus vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako