• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 21-Machi 27)

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:11:42

    Idadi ya maambukizi corona Rwanda yafika 50

    Wiki hii Serikali ya Rwanda ilitangaza visa vipya 13 vya ugonjwa wa Covid-19 chini ya wiki mbili tangu mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na ugonjwa huo na sasa idadi ya maambukizi imefikia 50.

    Kati ya maambukizi hayo, watano walikuwa wametokea Dubai,mmoja ametokea Netherlands na mmoja ametokea Marekani na wote hao walikuwa karantini wakati walipowasili. Wawili wanadaiwa kuambukizwa wakiwa ndani ya nchi.

    Rwanda imeweka vituo vitatu vya afya vya kupima maambukizi ya corona, viwili vikiwa Kigali na kingine kikiwa kusini mwa nchi hiyo.

    Wagonjwa wengi wa corona ambao wanatibiwa wanaonekana kupata nafuu nchini humo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako