• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei2-Mei 8)

    (GMT+08:00) 2020-05-08 19:36:23

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa virusi vya Corona unaweza kusababisha vifo kwa Waafrika wapatao 190,000 ndani ya mwaka mmoja

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa virusi vya Corona unaweza kusababisha vifo kwa Waafrika wapatao 190,000 ndani ya mwaka mmoja tangu uanze, kama ukishindwa kudhibitiwa.

    Mkurugenzi wa WHO-Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amesema kuna uwezekano kuwa virusi vya Corona haitosambaa kwa kasi barani humo kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine duniani.

    Hata hivyo, amezitaka Serikali kuweka mikakati ya kupima virusi hivi, kuwatibia wagonjwa, kuweka wenye maambukizi karantini na vilevile kutafuta wale waliokuwa karibu na wagonjwa wa Virusi hivyo.

    Awali, WHO ilitabiri Waafrika Milioni 29 hadi 44 wanaweza kupata virusi hivi

    kwa mwaka mmoja na Milioni 5.5 wanaweza kuhitaji tiba Hospitali, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa sekta za afya katika nchi nyingi.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako