• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 9-Mei 15)

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:33:10

    Wafanyakazi Twitter waruhusiwa kufanyia kazi nyumbani daima

    Kampuni ya Twitter imewaambia wafanyakazi wake kwamba wanaweza kufanyia kazi nyumbani "daima" kama wanataka kufanya hivyo wakati ikitathmini hali ya baadae ya mtandao huo wa kijamii baada ya janga la virusi vya corona.

    Uamuzi huo umekuja huku kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii ukisema kuwa hatua zake za kufanyia kazi nyumbani wakati wa hamri ya kukaa nyumbani zimekua za mafanikio.

    Lakini pia imesema kuwa itawaruhusu wafanyakazi kurejea ofisini iwapo watachagua kufanya hivyo itakapofungua ofisi zake.

    Mapema wiki hii, Google na Facebook zilisema kuwa wafanyakazi wake wanaweza kufanyia kazi nyumbani hadimwishoni mwa mwaka huu.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako