• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 9-Mei 15)

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:33:10

    Afisa aliyetemewa mate na mtu mwenye Covid-19 afariki

    Afisa anayekatisha tiketi amefariki baada ya kutemewa mate na mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa alikuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

    Belly Mujinga, 47, ambaye alikuwa na matatizo ya kupumua, alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Victoria jijini London mwezi Machi alipodhalilishwa, sambamba na mfanyakazi mwenzie wa kike.

    Ndani ya siku kadhaa baada ya tukio hilo, wanawake wote waliugua ugonjwa wa corona

    Polisi wamesema kuwa madai yamefunguliwa ili kumtafuta mwanaume aliowatemea mate wanawake hao wawili.

    Bi. Mujinga alikuwa kwenye kituo hicho tarehe 22 mwezi Machi wakati alipokabiliwa na mshukiwa huyo.

    Mumewe Lusamba Gode Katalay alisema mwanaume huyo alimuuliza mke wake alikuwa akifanya nini pale. Mshukiwa alikiri kuwa alikuwa na virusi vya corona kabla ya kuwatemea mate na kutoweka.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako