• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 16-Mei 22)

  (GMT+08:00) 2020-05-22 21:13:03
  Mawaziri wengi zaidi waambukizwa Corona Sudan Kusini

  Mawaziri 10 nchini Sudan Kusini wanadaiwa kuambukizwa virusi vya corona nchini humo.

  Waziri wa Habari wa Sudani Kusini Michael Makuei anadaiwa kunukuliwa akisema kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na corona nchini humo.

  Miongoni mwa mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hajakutwa na maambukizi.

  Inaripotiwa kuwa mawaziri hao wamepata maambukizo baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona.

  Mawaziri wote 10 wamejitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya.

  Taarifa za kuambukizwa kwa mawaziri hao zinakuja siku chache baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar kutangaza kuwa amekutwa na virusi pamoja na mkewe, ambaye ni Waziri wa Ulinzi.

  Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo pia wanadaiwa kuambukizwa virusi na kwa sasa wapo karantini.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako