• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 16-Mei 22)

    (GMT+08:00) 2020-05-22 21:13:03

    Burundi yakamilisha uchaguzi wa urais salama licha ya changamoto za janga la Corona

    Shughuli ya upigaji kura nchini Burundi ilimalizika salama na kwa utulivu siku ya alhamisi , licha ya fukuto la machafuko ya kisiasa na janga la virusi vya corona huku upinzani nao ukiituhumu mamlaka kwa udanganyifu. Wakati uchaguzi ukionekana kama uchaguzi wa kwanza wa ushindani nchini humo tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka 1993, mgombea wa chama tawala, CNDD-FDD, Jenerali mstaafu Evariste Ndayishimiye ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho akichuana na kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa na vyama vingine vitano.

    Rais Pierre Nkrunziza anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa miaka 15. Uchaguzi huo unafanyika wakati ambapo Burundi imeripoti visa 42 vya maambukizi na kifo kimoja. Kwa mujibu wa taasisi ya kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika, ni watu 633 tu nchini humo wamepimwa virusi vya corona. Mamlaka zilisema ilikuwa salama kwa uchaguzi kuendelea licha ya maradhi hayo na kuwataka Warundi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako