• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 29-Septemba 4)

    (GMT+08:00) 2020-09-04 15:29:04

    Wizara ya Afya kuchapisha zabuni zote za Corona – Rais Kenyatta

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamuru Wizara ya Afya kuchapisha zabuni zote zinazohusiana na jinsi serikali ilivyoshughulikia janga la Covid-19. Zabuni zinazotakiwa kuchapishwa ni zile zilizotolewa na mamlaka ya usambazaji vifaa vya matibabu nchini Kenya (Kemsa).

    Amri ya rais inafuatia madai ya ubadhirifu wa fedha za umma uliokumba mchakato wa kutolewa kwa zabuni hizo. Wabunge wameanza uchunguzi binafsi kuhusiana na madai hayo. Afisa mkuu mtendaji wa Kemsa wiki iliyopita alifahamisha kamati ya bunge la seneti kwamba alipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na katibu mkuu katika wizara hiyo Susan Mochache kuhusu jinsi ya kutoa zabuni hizo.

    Wawili hao wamesema hawajafanya kosa lolote.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako