• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 29-Septemba 4)

    (GMT+08:00) 2020-09-04 15:29:04

    Rais wa Ufaransa awapa onyo viongozi Lebanon

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewapa wanasiasa wa Lebanon hadi mwisho mwa mwezi Oktoba kuanza kutekeleza mageuzi, akisema msaada wa kifedha utazuiwa na baadaye kuwekewa vikwazo kama rushwa itazuia mchakato huo.

    Macron aliuambia mkutano wa wanahabari mjini Beirut kuwa viongozi wa kisiasa wamekubali kuunda serikali ya wataalamu katika wiki mbili zijazo kusaidia kuliweka kwenye mkondo sahihi taifa hilo la Mashariki ya Kati linalozidiwa na uzito wa mporomoko wa kiuchumi.

    Macron amesema Paris iko tayari kusaidia kuandaa na kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa na Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba. Rais huyo wa Ufaransa amesema vikwazo huenda vikatangazwa kama kutakuwa na ushahidi wa rushwa na vitaratibiwa na Umoja wa Ulaya, lakini hiyo sio mada ya Oktoba kwa sababu kwa sasa wapo katika mchakato wa kuaminiana na kushirikiana. Katikati ya mji mkuu Beirut, polisi ya kukabiliana na ghasia na magari ya ulinzi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji nje ya bunge waliokasirishwa na wanasiasa.

    Macron alitembelea eneo la bandari lililokumbwa na mlipuko uliowauwa karibu watu 190 na akasema anataka ahadi halali za mpango wa mageuzi, ambao unajumuisha ukaguzi wa mahesabu ya benki kuu, na utaratibu wa kufuatilia, ukiwemo uchaguzi wa bunge katika miezi sita hadi 12. Rais huyo wa Ufaransa amesema alijaribu kuwashawishi wanasia kuwa sheria ya uchaguzi hazipaswi kuwa utangulizi wa mageuzi kwa sababu itasitisha kila kitu.

    Shinikizo kutoka kwa Macron, ambaye alisema ataitembelea tena nchi hiyo Desemba, tayari imevisukuma vyama vikuu vya kukubaliana kuhusu waziri mkuu mpya, Mustapha Adib, ambaye ametoa wito wa kuundwa haraka kwa serikali na kuahidi kuyatekeleza haraka mageuzi ili kufikia makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF. Katika siku za nyuma, kuunda baraza la mawiri kulichukua miezi kadhaa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako