• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 29-Septemba 4)

    (GMT+08:00) 2020-09-04 15:29:04

    Makubaliano ya kihistoria yaafikiwa baina ya pande hasimu Sudan

    Mnamo siku ya Jumatatu wiki hii, viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan na wakuu wa makundi ya waasi katika jimbo la Darfur , waliafikia makubaliano ya kihistoria ya mkataba wa amani unaoelezewa ni hatua muhimu ya kwanza kuelekea katika kumaliza vita vya takriban miaka 17.

    Kupatikana kwa amani na waasi ni hatua muhimu sana kwa serikali ya mpito ya Sudan ambayo imeingia madarakani miezi kadhaa baada ya kuuangusha utawala wa Bashir April 2019.

    Viongozi wa muungano wa makundi ya waasi, Sudan Revolutionary Front (SRF) kutoka jimbo la magharibi la Darfur na majimbo ya kusini ya Kordofan Kusini na Blue Nile waliinua juu mikono yao kama njia ya kusherekea kupatikana kwa mkataba huo.

    Mkataba huo ulipendekezwa awali lakini haukusainiwa kama njia ya kuacha mlango wazi kwa makundi mawili muhimu ya waasi kujiunga kwenye makubaliano ya mwisho, maafisa wamesema.

    Makundi mawili ya waasi yalikataa kushiriki katika makubaliano hayo. Wakiwa na hamasa kubwa kusheherekea mafanikio tangu kuangushwa kwa dikteta wa muda mrefu Omar al Bashir mwaka 2019 na kuundwa serikali ya mpito, viongozi wa Sudan walikutana katika mji mkuu wa Sudan kusini wa Juba.

    Kusukuma mbele amani na waasi limekuwa suala lililopewa kipaumbele na serikali ya mpito ilioingia madarakani baada ya kuangushwa utawala wa Bashir mwezi April mwaka 2019.

    Umoja wa Mataifa (UN) unasema takriban watu laki 3 waliuawa huko Darfur tangu waasi walipoamua kuchukua silaha mwaka 2003. Mzozo katika jimbo la Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile ulizuka mwaka 2011, baada ya Sudan kusini kujipatia uhuru, na hivyo kuanzisha tena vita vya miongo miwili.

    Mkataba uliofikiwa Jumatatu unazingatia masuala makuu ya usalama, umiliki wa ardhi, mfumo wa mpito wa sheria, kushirikiana madaraka, na kurejea nyumbani kwa watu waliohama makazi yao kwa sababu ya mapigano.

    Pia unapendekeza kuvunjwa kwa makundi ya waasi na kushirikisha wapiganaji wao kwenye jeshi la taifa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako