• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 19-Septemba 25)

    (GMT+08:00) 2020-09-25 16:14:40

    Waziri wa ulinzi Mali awa rais wa mpito

    Mali imewatangaza viongozi wa serikali mpya ya mpito, ambao wataweza kuendeleza mahusiano madhubuti na jeshi pamoja na uwepo wa shinikizo la kimataifa la kuteuliwa kwa kiongozi raia baada ya mapinduzi ya kijeshi.

    Katika taarifa yake ilioneshwa kwa njia ya video, kiongozi wa kijeshi Kanali, Assimi Goita amesema Waziri wa zamani wa ulinzi Bah Ndaw, atakuwa Rais wa serikali ya mpito wakati yeye mwenyewe atahudumu kama makamo wa rais.

    Tangazo hilo limetolewa baada ya juma lililopita Jumiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi yenye mataifa 15 wanachama ECOWAS kutoa siku kwa watawala wa kijeshi wa Mali kuwateuwa viongozi wa kiraia, ikionya kwamba haitaviondoa vikwazo vyake endapo hatua hiyo haitotekelezwa.

    Vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo ni marufuku ya kibiashara na kufunga mipaka, katika kipindi ambacho kilizongwa na mapinduzi ya Agosti 18, ambayo yalimuondoa mamulakani Rais Ibrahim Boubakar Keita.

    Hata hivyo watawala wa kijeshi juma lililpita walisema wangependelea jeshi kuongoza serikali ya mpito. Katika taarifa yake ya Jumatatu Goita amesema Ndaw, mstaafu mwenye umri wa miaka 70, ametuliwa na kuwa rais wa mpito na jeshi, na kuongeza kuwa kila pendekezo lililotolewa lina faida na hasara zake, akitolea mfano uteuzi kati ya rais raia na mwanajeshi. Hata hivyo aliongeza kusema kamati ya uteuzi ilizingatia matakwa ya ulimwengu katika chagua lililofanyika.

    Ndaw ambae aliwahi kuwa rubani wa helikopta, ambae pia alikuwa msaidizi wa kambi ya diktekta wa zamani Mali, Muossa Traore, ambea alifariki dunia juma lililopita akiwa na umri wa miaka 83.

    Kwa mujibu wa masuala yalioibuka katika kongamano hilo ni pamoja na uwepo wa rais wa mpito ambae ataongoza kwa miezi 18 kabla ya kupatikana kwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa taifa hilo. Uteuzi wa Ndaw umegawanya mawazo nchini Mali.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako