• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 31-Novemba 6)

    (GMT+08:00) 2020-11-06 16:54:56
    Magufuli aapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa kipindi cha pili

    John Pombe Magufuli aliapishwa rasmi kuwa rais wa Tanzania kwa awamu ya pili.

    Rais Magufuli alitetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28.10.2020.

    Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

    Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

    Baada ya kuapishwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma nchini Tanzania.

    Rais John Magufuli alitoa shukrani kwa Watanzania wote kwa kumuamini na kumchagua kwa mara nyingine kuliongoza taifa hilo kwa miaka mingine mitano.

    Katika hotuba yake amesisitiza kuwa ushindi aliopata si wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM) bali ni ushindi kwa Watanzania wote.

    Pia ameipongeza Tume ya uchaguzi Tanzania (NEC) kwa kusimamia vyema uchaguzi huo.

    Rais John Magufuli amesisitiza kwamba sasa uchaguzi umekwisha na kuwa jukumu kubwa ni kuendeleza jitihada za kuleta maendeleo katika taifa hilo na kuahidi kushirikiana na watanzania wote bila kujali itikadi na utofauti wao.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako