• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 7-Novemba 13)

    (GMT+08:00) 2020-11-12 20:35:19
    Mfumo wa reli mjini Nairobi kupunguza msongamano wa magari

    Nchini Kenya serikali imezindua mfumo mpana wa usafiri wa umma kusaidia kupunguza msongamano wa magari katika mji mkuu Nairobi.

    Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesema kwenye uzinduzi wa mfumo huo wa reli kwamba kutakuwa na upanuzi wa awamu kadhaa ili kufikia maeneo mengi ya mji na viunga vyake.

    Mjini Nairobi, kama miji mikuu mingi kote duniani, unazongwa na tatizo la msongamano wa magari, hasa asubuhi na jioni wakati wa pilka za kwenda kazini na kurejea nyumbani.

    Kuwepo kwa magari mengi na barabara nyembamba inamaanisha wakaazi wanatumia muda mwingi barabarani.

    Lakini sasa kufuatia kuzinduliwa kwa huduma ya usafiri wa reli, shinikizo barabarani inatajiwa kupungua.

    Mfumo huo mpya wa usafiri utawezesha wasafiri kuabiri treni hizo mpya kwenye vituo mbalimbali ambavyo pia vimeunganishwa na huduma ya mabasi ya mwendo kasi.

    Maeneo yanayonufaika moja kwa moja ni kama vile katikati mwa jiji, Kikuyu, Kitengela, Thika, Syokimau na Embakasi.

    Rais Uhuru Kenyatta anaupongeza mfumo huu wa usafiri kama wenye kuinua hadhi ya mji na uchumi kwa jumla.

    'Leo ni mwanzo mpya kwa mji wa Nairobi na viunga vyake. Kupitia juhudi hizi tunarejesha hadhi ya mji wetu mkuu na watu wake. Pia tuongeza umaarufu wetu kama lango kuu la kanda ya Afrika Mashariki na kati. Tuna kila sababu ya kujivunia mji wetu ambao sasa unaongoza kivitendo barani Afrika, kwa kuimarisha mifumo yake ya usafiri wa umma. Tunaleta suluhu za haraka kwa biashara wakati huo huo tukilinda mazingira yetu. Kwa jumla tunaboresha maisha kwa wakaazi wa Nairobi na wageni'

    Kulingana na taakwimu za mamlaka ya kitaifa ya usafiri NTSA, Mji wa Nairobi utakuwa na magari zaidi ya milioni 1.35 ifikapo mwaka 2030 na kwa wastani kila mwaka magari mapya 90,000 hununuliwa kila mwaka mjini humo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako