Matukio ya udanganyifu yatokea mara kwa mara kwenye miadi kupitia Mtandao wa Internet
2020-08-20 17:01:01| CRI

Matukio ya udanganyifu yatokea mara kwa mara kwenye miadi kupitia Mtandao wa Internet

Wakati wa janga la virusi vya Corona, watu wengi wanatafuta wapenzi kupitia mtandao wa Internet. Nchini China kuna APP mbalimbali zinazotoa huduma kama hizo, na kutokana na takwimu zilizotolewa na Tovuti ya Zhenai, katika miezi minne ya mwanzo mwaka huu, zaidi ya watu elfu 20 walipata wapenzi kupitia APP ya kampuni hiyo. Lakini wakati huo huo baadhi ya watu wanaona kuna hali ya udanganyifu kwenye App aina hiyo.

Kwenye App ya kutafuta wapenzi, watu wa pande tatu wakiwemo wanamke, wanamume na makuwadi wanakutana kwa njia ya video inayotangazwa kwa uwazi. Watumiaji wa mtandao wa Internet wakiingia kwenye "chumba" kupitia App hiyo wanaweza kutazama hatua yote ya Blind date bila malipo, na kuwadi atawaalika kuweka miadi.

Bw. Gao aliyejaribu kutumia APP ya aina hiyo alilalamika kuwa, lengo la upande wa wanawake kwenye APP hiyo ni kuomba zawadi, na wanaume wanapaswa kutozwa gharama kwa kufanya urafiki na kuwasiliana na wanawake, na tayari alitumia zaidi ya yuan mia tano, sawa na dola za kimarekani 70 kwa wiki. Kwa maoni yake, matumizi ya fedha si suala kubwa, tatizo halisi ni kwamba lengo la watu wengi hawana na moyo wa dhati wa kutafuta wapenzi, na wengine ni wadanganyifu.

Mbali na hayo, kutokana na kuwa watu wanaweza kujiandikisha kwenye App kwa njia rahisi kwa kuandaa habari za jinsia, umri na kiwango cha elimu tu, hali ambayo inatoa fursa kwa baadhi ya watu kufanya uhalifu. Hivi karibuni polisi ya mji wa Xinzhou ya Mkoa wa Shanxi imeshughulikia kesi zaidi ya 30 za udanganyifu kupitia App ya kutafuta wapenzi ambazo zinahusisha zaidi ya dola za kimarekani laki 7. Bibi Li ambaye alijiandikisha kwenye jukwaa moja la kutafuta wapenzi, alidanganywa na kupata hasara ya fedha za dola za kimarekani elfu 34.