China yaitaka Marekani iache kukandamiza TikTok
2024-03-15 08:50:16| CRI

China imetoa wito kwa Marekani kukomesha ukandamizaji usio na sababu dhidi ya makampuni kutoka nchi nyingine, kufuatia mswada wa Marekani unaolenga programu ya video fupi ya TikTok.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China He Yadong amesema Marekani inapaswa kuheshimu kwa udhati uchumi wa soko huria na kanuni ya ushindani wa haki, na kutoa mazingira ya wazi, ya haki na yasiyo ya kibaguzi kwa makampuni kutoka nchi zote. Amesema pande husika zinapaswa kutii sheria na kanuni za China, na China itachukua hatua zote muhimu ili kulinda kwa uthabiti haki na maslahi yake halali.

Mapema wiki hii, Baraza la Wawakilishi la Marekani liliidhinisha mswada ambao ungehitaji TikTok kuachana na kampuni yake mama, kampuni kubwa ya kiteknolojia ya China ya ByteDance, au kukabiliwa na marufuku ya nchi nzima nchini Marekani.