China na Tanzania zaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi
2024-04-16 08:16:44| CRI

China na Tanzania jana Jumatatu ziliandaa tafrija mjini Dar es Salaam kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Sherehe hizo zilizoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Bw. Januari Makamba na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Chen Mingjian, zilihudhuriwa na Wachina walioko nchini Tanzania na maofisa wa serikali ya Tanzania.

Waziri Makamba amesema urafiki kati ya nchi hizo mbili umepitia majaribu ya wakati na uhusiano umeimarika zaidi leo.

Kwa upande wake, Balozi Chen amesema, miaka 60 iliyopita ni kipindi cha mshikamano na umoja kati ya China na Tanzania, ambapo nchi hizo mbili zimesaidiana na kuungana mkono, na kuwa na ushirikiano wa dhati, maendeleo ya pamoja, na mawazo ya pamoja.