Marais wa China na Sierra Leone wafanya mazungumzo
2024-02-29 09:02:22| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone ambaye yuko ziarani nchini China.

Kwenye mazungumzo yao rais Xi ameeleza kuwa China inapenda kushirikiana na Sierra Leone kuimarisha kuaminiana kisiasa katika kiwango cha juu, kuhimiza ushirikiano wa kiutendaji wa kusaidiana, kuongeza uratibu kwenye mambo ya kikanda na kimataifa, ili kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kupanda katika ngazi ya juu zaidi.

Pia amesema China itaimarisha ushirikiano wa kirafiki na nchi za Afrika, kuunga mkono maendeleo ya viwanda barani Afrika, mpango wa mambo ya kisasa wa Afrika, mpango wa ushirikiano wa kuwaandaa wataalamu kati ya China na Afrika, na Ajenda ya Mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, kuunganisha vizuri mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali za Afrika, na kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye kiwango cha juu, ili kuhimiza dunia kupata mustakabali mzuri wenye amani, usalama, ustawi na maendeleo.

Rais Bio amesema Sierra Leone inaishukuru China kwa uungaji mkono mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo, pia amepongeza maendeleo makubwa yaliyopatikana na wananchi wa China chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China.