Mama Atangaza jinsi Anavyofuma Sweta
2020-08-25 13:26:56| CRI

Mama Atangaza jinsi Anavyofuma Sweta

Kutokana na biashara kutomwendea vizuri katika miaka kadhaa iliyopita, mwaka 2018, mmiliki mmoja wa duka kwenye mtandao wa Tmall Bi. Zhang Ka aliyezaliwa miaka ya 70, alifungua mlango wa kutangaza biashara yake mara kwa mara kupitia jukwaa la Taobao la mtandaoni. Hivi sasa kikundi cha wafumaji sita, akiwemo yeye, wanaotangaza moja kwa moja jinsi wanavyofuma sweta kupitia mtandao wa internet, wameweza kuuza nyuzi za kufumua zenye thamani ya yuan milioni kumi, ambazo ni sawa na dola za kimarekani milioni 1.43, ndani ya nusu mwaka, mapato ambayo yameongezek mara ishirini kuliko zamani.

Kwenye chumba cha kutangazia cha Bibi Zhang Ka, huwa anakaa katikati ya chumba na kufuma sweta kimyakimya, lakini hivi sasa matangazo yake kwa wastani yanaweza kuvutia watazamaji zaidi ya elfu 30.

Hadi sasa, kikundi cha mama wafumaji cha Bibi Zhang Ka kimekuwa na watu sita. Wafumaji hao wenye umri wa wastani wa 50 wanafanya matangazo ya moja kwa moja kwa masaa yasiyopungua 12 kila siku, na karibu mauzo yote ya nyuzi yanafanyika kwenye kipindi cha matangazo. Haswa katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya Corona, biashara ya Bibi Zhang Ka imeongezeka kwa kiasi kikubwa, na mapato yake yalifikia yuan milioni kumi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, na anakadiria kuwa yatafikia milioni ishirini kwa mwaka mzima, ikilinganishwa na milioni moja ya mwaka 2017 kabla ya kufungua matangazo ya mtandaoni.