Majukwaa ya usambazaji wa vyakula yatoa mipango ya kupunguza matumizi ya kupita kiasi ya vyakula
2020-09-14 16:41:04| CRI

Majukwaa ya usambazaji wa vyakula yatoa mipango ya kupunguza matumizi ya kupita kiasi ya vyakula

Ripoti kuhusu matumizi ya kupita kiasi ya vyakula katika miji ya China imeonesha kuwa, hivi sasa hali ya matumizi ya kupita kiasi ya vyakula ni mabaya zaidi kwenye migahawa, watalii, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari… Kutokana na hali hii, majukwaa mbalimbali ya usambazaji wa vyakula ya China yametoa mipango ya kubana matumizi ya vyakula.

Mwezi Agosti, Kampuni ya Meituan ya Beijing ikishirikiana na mashirika mbalimbali nchini zikiwemo Shirikisho la biashara la China, na Shirika la upikaji wa vyakula zimetoa wito kwa migahawa kusimamisha vitendo vya kutumia kwa kupita kiasi matumizi ya vyakula, ambapo zitatoa maelekezo kuhusu radha na kiasi cha vyakula, ili kuwarahisisha wateja wafanya oda inayolingana na mahitaji yao, na kuepukana na matumizi kupita kiasi ya vyakula.

Mbali na hayo, mashirikisho ya migahawa ya sehemu mbalimbali pia yamejiunga na operesheni hiyo, na kutoa sahani ya nusu vyakula au mpango wa "N-1", kwa mfano mgahawa utaandaa vyakula vinavyowafaa watu tisa kwa wateja kumi wa jumla.

Zaidi ya hayo, ili kuzuia hali ya matumizi ya kupita kiasi ya vyakula kwenye mtandao wa kijamii, majukwaa yanayojulikana ya video nchini China zikiwemo "Dou Yin" na "Kuai Shou" yameimarisha ukaguzi juu ya video zinazohusu vyakula.