Rais Xi Jinping ahudhuria na kuhutubia mkutano wa 16 wa kilele wa BRICS
2024-10-24 10:11:55| cri

Rais Xi Jinping wa China Jumatano asubuhi alihudhuria na kuhutubia mkutano wa 16 wa viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika katika kituo cha mikutano cha Kazan nchini Russia.

Katika hotuba yake Rais Xi amebainisha kuwa upanuzi wa BRICS ni hatua muhimu katika historia ya maendeleo ya jumuiya hiyo, na pia ni tukio muhimu linaloashiria mabadiliko ya muundo wa kimataifa. Kujumuika kwa nchi za BRICS kunatokana na azma ya pamoja, na kunaendana na mwelekeo mkuu wa dunia wa kuelekea amani na maendeleo.

Rais Xi ametoa mapendekezo matano kuhusu maendeleo ya BRICS katika siku zijazo, akiitaka jumuiya ya BRICS iwe mlinzi wa usalama wa pamoja, mtangulizi wa maendeleo yenye ubora, mtekelezaji wa maendeleo endelevu, mwongozaji wa mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia, na mtetezi wa mapatano na maingiliano kati ya staarabu tofauti.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na wenzake wa BRICS katika kufungua hali mpya ya maendeleo yenye ubora wa juu, na kusukuma kwa pamoja ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.