Rais Xi Jinping wa China Alhamisi alihudhuria mazungumzo ya viongozi wa “BRICS Plus” katika siku ya mwisho ya mkutano wa kilele wa BRICS mjini Kazan, akisema ataunga mkono Nchi za Kusini.
Kwenye mazungumzo hayo, Xi amesema kuinuka kwa pamoja kwa Nchi za Kusini ni ishara ya wazi ya mabadiliko makubwa duniani. Nchi nyingi zaidi za Kusini zinakaribishwa kushiriki kwenye mambo ya BRICS kupitia kuwa nchi wanachama rasmi, nchi washirika, au mfumo wa “BRICS Plus”, ili kuunganisha nguvu kubwa ya Nchi za Kusini na kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Ameongeza kuwa China siku zote inaweka Nchi za Kusini moyoni na kuziunga mkono bila kujali kuna mabadiliko gani duniani.
Viongozi kutoka Asia, Afrika, Mashariki ya Kati na Latin Amerika pamoja na wajumbe wa mashirika mengi ya kimataifa walihudhuria kwenye mkutano huo, ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres.