Asubuhi ya Tarehe 18, Novemba kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China katika wakati wa kuhudhuria kwenye kipindi cha kwanza chaMkutano wa 19 wa kundi la nchi 20 (G20) huko Rio de Janeiro, Brazil. (Picha na Li Xueren/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China amesema China ingependa kushirikiana na pande zote ili kujenga dunia yenye maendeleo kwa pamoja, na ametoa hatua nane za China kwa ajili ya maendeleo ya dunia.
Xi ameyasema hayo Jumatatu kwenye Mkutano wa 19 wa kundi la nchi 20 (G20) kuhusu Mapambano dhidi ya Njaa na Umaskini. Katika hotuba yake yenye kichwa "Kujenga Dunia yenye Maendeleo kwa Pamoja," Xi alidokeza kuwa mabadiliko ya kiwango ambacho hakijaonekana katika miaka mia moja iliyopita sasa yanaongezeka kote duniani, na binadamu wanakabiliwa na fursa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa.
Ameeleza kuwa mafanikio ya China yamethibitisha kwamba nchi zinazoendelea zinaweza kuondokana na umaskini, akitoa mfano kwamba “ndege mnyonge anaweza kuanza kuruka mapema na juu zaidi, unapokuwepo uvumilivu, ustahamilivu, na moyo wa kujitahidi ambao huwezesha matone ya maji kupenya ndani ya miamba baada ya muda na kubadilisha mwongozo kuwa hali halisi”.
Amesisitiza kuwa kama China imeweza kupata mafanikio , nchi nyingine zinazoendelea pia zinaweza kufanikiwa , na huu ni umuhimu wa mapambano ya China dhidi ya umaskini kwa Dunia.