Jicho Mwanamume afungwa kwa kujaribu kumchoma mwanamke kwa sindano yenye virusi vya HIV
2020-09-16 16:03:51| CRI

Jicho Mwanamume afungwa kwa kujaribu kumchoma mwanamke kwa sindano yenye virusi vya HIV

Mwanamume aliyeambukizwa Ukimwi kutoka mkoa wa Shandong amehukumiwa kifungo cha miezi 18 kwa kupanga kumchoma mwanamke kwa kutumia sindano yenye virusi vya HIV baada ya mwanamume mmoja kumtaka afanye hivyo kwa malipo.

Mwanamume huyo anayeitwa Shen Shizhuang mwenye umri wa miaka 31, aligunduliwa kuwa na virusi vya Ukimwi mwaka 2015. Aliweka tangazo kwenye mtandao wa Internet mwezi Septemba mwaka jana, akisema anaweza kuwasaidia watu kukusanya madeni au kulipiza kisasi kwa kusambaza virusi vya HIV kwa wengine.

Baada ya kusoma tangazo hilo, Bw. Huang Zhichao aliwasiliana na Shen Zhizhuang na kumlipa yuan elfu 20, sawa na dola za kimarekani elfu 2.9, kama nauli ya kusafiri kwenda mkoa wa Guangxi, ili kumchoma shindano yenye virusi vya Ukimwi binti ya mtu anayeitwa Zhong kama kitendo cha kulipiza kisasi.

Kwa bahati nzuri Bw. Shen alikamatwa mjini Guilin, mji uliopo Guangxi, kabla ya kutekeleza mpango wake, na kuhukumiwa kifungo cha miezi 18 kwa kuhatarisha usalama wa umma.