Chombo cha China kinachochunguza sayari ya mwezi Chang’e chaanza kazi katika siku ya 24 ya mwezi
2020-11-10 19:17:27| cri

Chombo cha China kinachochunguza sayari ya mwezi Chang’e chaanza kazi katika siku ya 24 ya mwezi

Chombo cha China kilichotua na kinazunguka kufanya utafiti kwenye sayari ya mwezi kimeanza kazi kwa siku ya 24 ya mwezi kwenye upande wa mbali wa mwezi.

Kituo cha utafiti wa mwezi na utafiti wa anga ya juu cha Idara ya Anga za Juu ya China CNSA, kimesema vyombo hivyo viliamka jumatatu kwa nyakati tofauti. Mchana mmoja kwa mwezi ni sawa na siku 14 za dunia, na usiku mmoja ni sawa na siku 14 pia. Kwa mujibu wa data zilizochukuliwa kutoka kwenye chombo hicho, wanasayansi wa China wamefanya magunduzi mapya.