Rais Xi Jinping ahutubia Mkutano wa kuadhimisha miaka 30 ya kuendelezwa na kufungua mlango kwa eneo la Pudong mjini Shanghai
2020-11-12 19:47:27| cri

Rais Xi Jinping ahutubia Mkutano wa kuadhimisha miaka 30 ya kuendelezwa na kufungua mlango kwa eneo la Pudong mjini Shanghai

Mkutano wa kuadhimisha miaka 30 ya kuendelezwa na kufungua mlango kwa eneo la Pudong umefanyika leo asubuhi mjini Shanghai. Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo. 

Kwenye hotuba yake, Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa miaka 30 iliyopita, kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China ilitoa uamuzi muhimu wa kuendeleza na kufungua mlango kwenye eneo la Pudong mjini Shanghai, na kufungua ukurasa mpya wa kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango nchini China. Baada ya kuingia kwenye zama mpya, kamati kuu ya Chama imelitaka eneo la Pudong liendelee kuendelezwa na kupewa majukumu mbalimbali ya mikakati ya taifa.

Rais Xi amebainisha kuwa katika miaka 30 iliyopita, eneo la Pudong limetekeleza kwa njia za kivumbuzi maamuzi na mipango iliyowekwa na Kamati kuu ya Chama, na kupata mafanikio makubwa yanayong’ara kote duniani, ambayo yamethibitisha wazi nguvu bora ya mfumo wa usoshalisti wenye umaalumu wa China. Rais Xi Jinping anasema:

“Uzoefu wetu umethibitisha kuwa nadharia, njia na mikakati ya msingi ya Chama iliyowekwa tangu mkutano wa tatu wa kamati kuu ya awamu ya 11 ya Chama ni sahihi; mageuzi na ufunguaji mlango ni njia ya lazima ya kushikilia na kuendeleza ujamaa kwenye umaalum wa China na kutimiza uhuishaji wa taifa la China; mageuzi na maendeleo yanatakiwa kuzingatia maslahi ya umma na kuyafanya kuwa kiini chake, na kuyafanya matarajio ya wananchi kuwa na maisha bora kuwa lengo letu, na tunapaswa kuwategemea wananchi ili kufanikisha jukumu letu kubwa la kihistoria.”

Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesisitiza haja na umuhimu wa kuhimiza uvumbuzi, na kutoa msukumo mpya kwa maendeleo yenye ubora wa hali ya juu. Pia ameitaka China isukume mbele ufunguaji mlango wa kimfumo wa kiwango cha juu, kujenga nguvu bora mpya kwenye ushirikiano na ushindani wa kimataifa, na kuimarisha uwezo wa kuhamasisha raslimali za dunia, ili kuhudumia muundo mpya wa maendeleo ya China.

Rais Xi amesisitiza kuwa, mwaka kesho China itaadhimisha miaka 100 ya Chama cha kikomunisti cha China, na Shanghai ndiko ni chimbuko la Chama chetu. Amekitaka Chama kiendelee kuinua kiwango na ubora wa ujenzi wake, na kuhakikisha mwelekeo sahihi wa mageuzi na ufunguaji mlango. Anasema:

“Shanghai ni mji wa heshima, na pia ni sehemu inayoendelea kushuhudia miujiza, Katika miaka 30 iliyopita tangu eneo la Pudong lilipoanza kuendelezwa na kufungua mlango, tumefuata njia ya kukomboa mawazo na kuimarisha mageuzi, ni njia ya kuikumbatia dunia na kupanua ufunguaji mlango, na pia ni njia ya kivumbuzi ya kusonga mbele. Tukitupia macho siku za baadaye, tuna kila sababu za kuamini kuwa kwenye njia ndefu ya kutimiza maendeleo ya China katika zama mpya, mji wa Shanghai hakika utaleta miujiza mipya inayong’ara duniani, na hakika utaonesha hali mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa.”