Zaidi ya bidhaa mpya na teknolojia 2,500 zazinduliwa katika maonyesho ya teknolojia ya juu ya China
2020-11-16 18:39:30| cri

Zaidi ya bidhaa mpya na teknolojia 2,500 zazinduliwa katika maonyesho ya teknolojia ya juu ya China

Maonyesho ya 22 ya Teknolojia ya Juu ya China (CHTF) yamemalizika jana jumapili katika mji wa Shenzhen, huku bidhaa mpya 1,790 na teknolojia mpya 767 zikizinduliwa.

Waandaaji wa maonyesho hayo yenye kaulimbiu “Kubadilisha Siku za Baadaye kwa Teknolojia na Kuchochea Maendeleo kwa Uvumbuzi” wamesema, watu zaidi ya 3,000 kutoka nchi na sehemu 53 pamoja na mashirika ya kimataifa walishiriki moja kwa moja na kwa njia ya mtandao.

Zaidi ya miradi 9,000 ya teknolojia ya juu ilionyeshwa kwenye maonyesho hayo, ikihusisha maeneo mbalimbali pamoja na teknolojia ya 5G, na akili bandia.

Maonyesho ya Teknolojia ya Juu ya China yalianzishwa mwaka 1999, na ni moja ya maonyesho makubwa ya teknolojia na yenye ushawishi mkubwa nchini China.