Roketi ya Long March-5 kurushwa mwishoni mwa mwezi Novemba
2020-11-17 18:30:46| CRI

Roketi ya Long March-5 kurushwa mwishoni mwa mwezi Novemba

Baada ya kazi ya kuunganisha roketi ya ya Long March-5 na chombo cha kuchunguza mwezi cha Chang’e-5 kukamilika, roketi hiyo imeinuka wima na kuhamishwa kwenye eneo la urushaji katika kituo cha kurushia vyombo vya anga za juu cha Wenchang, China, na inatarajiwa kurushwa kwa wakati mwafaka mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba.

Hii  itakuwa ni mara ya pili kwa roketi ya Long March-5 kutumika kurusha chombo cha anga ya juu, kabla ya hapo ilirusha kwa mafanikio chombo cha utafiti cha Tianwen-1 kwenda sayari ya Mars.