Uganda: Utendaji wa uchumi wa Uganda waimarikia
2020-11-19 18:52:42| cri

Ripoti mpya ya wizara ya fedha nchini Uganda inaonyesha  kuwa uchumi wa nchi hiyo unaendelea kurejea baada ya kipindi kigumu cha janga la COVID-19,

Ripoti ya utendaji wa kila mwezi ya Oktoba ilionyesha kuwa kwa mwezi wa nne mfululizo, Kiashiria cha Ununuzi (PMI) kimeendelea kupanda na kufikia zaidi ya alama 50.

Kiwango cha zaidi ya alama 50.0 ni ishara ya utendaji mzuri lakini chini ya hapo kinaonyesha kuzorota.

Wizara hiyo imesema kuboreka kwa hali ya uchumi kumechangiwa kuongezeka kwa mahitaji kufuatia kupunguza vizuizi, na kusababisha upanuaji zaidi katika pato na ajira.