Tanzania: Uhaba wa saruji waikumba Tanzania
2020-11-19 18:53:26| cri

Wilaya ya Nyasa imekumbwa na uhaba mkubwa wa Saruji hali iliyotokana na wafanyabiashara kuogopa kuingiza,  na kuuza kwa bei kali inayotokana na uadimikaji wa bidhaa hiyo katika viwanda vinavyozalisha.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mh. Isabela Chilumba, ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ya kikazi, katika maduka ya wafanyabiashara wa Saruji yaliopo Makao makuu ya Wilaya ya Nyasa Mjini Mbamba bay.

Chilumba amefafanua kuwa Lengo la Ziara hiyo ya Kikazi, akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama,  ilikuwa ni kuwabaini wafanyabiasha wanaouza Saruji kwa bei kubwa, na kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwa, kulikuwa na Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuwa kuna wafanyabiashara wameongeza bei kutoka Sh 16000 kwa mfuko hadi kufikia tsh 20,000.

Kampuni nne kubwa za kuzalisha saruji zimefungwa ili kufanyia ukarabati mashine zake.