Ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nguvu za maji cha Karuma, Uganda wakaribia kukamilika
2020-11-19 18:06:40| CRI

Ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji cha Karuma, Uganda kinachojengwa na kampuni ya Sinohydro ya China umeingia kwenye hatua ya mwisho bila kujali changamoto kubwa zinazotokana na janga la COVID-19.

Meneja wa mradi huo Bw. Deng Changyi hivi karibuni alisema mradi huo umekamilika kwa asilimia 98, na kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha megawati 600 za umeme kitakuwa kikubwa zaidi nchini Uganda.

Kituo cha Karuma kinajengwa juu na chini ya Mto Nile, wilaya ya Kiryandongo iliyoko magharibi mwa Uganda.