Tume ya uchaguzi ya Uganda yaonya kufutwa kwa kampeni za uchaguzi
2020-11-20 19:06:45| CRI

Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda jana imeonya kuwa huenda ikafuta kampeni za uchaguzi kama miongozo iliyotolewa itaendelea kukiukwa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Simon Byabakama amesema kwenye taarifa hiyo kuwa, wagombea wanapaswa kuacha kufanya mikusanyiko kwa njia inayokiuka miongozo ya kampeni.

Tume hiyo imesema, wagombea au wawakishili wao wameendelea kuhamasisha wafuasi wao kukusanyika kwa wingi katika maeneo ya kampeni, hali inayokiuka mwongozo wa kutofanya mkutano wa zaidi ya watu 200 kutokana na janga la COVID-19.