SOKA: Messi achoshwa na shutuma dhidi yake
2020-11-20 16:29:07| cri

Nyota wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Lionel Messi amesema amechoka maisha ya kulaumiwa kuwa ndiye chanzo cha matatizo ndani ya klabu hiyo. Messi ameyasema hayo jana alipowasili uwanja wa ndege akitokea nchini kwao Argentina alipokuwa na majukumu ya timu ya taifa. Maneno ya Messi kukiri kuchoshwa kulaumiwa kwa kila kitu ndani na kuwa huenda akaendelea kufikiria kutimka ndani ya Barcelona na kutafuta changamoto nyingine kwa kuungana na aliyekuwa kocha wake Pep Guadiola.