Shughuli za kibiashara zarudi katika hali ya kawaida Kampala na vitongoji vyake
2020-11-20 19:05:03| cri

Shughuli za kibiashara katika mji wa Kampala na vitongoji vyake zimeanza kurudi katika hali ya kawaida baada ya jeshi la polisi nchini humo kuimarisha hali ya usalama baada ya ghasi za kisiasa zilizokuwa zimetawala kwa siku kadha. Katika barabara kuu kama vile Jinja na Katwe askari wa polisi walionekana wakipiga doria na kuweka vizuizi ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Covid 19.

Baadhi ya sehemu ambazo zilishuhudia ghasia za kampeini za uchaguzi zilionekana zikiwa tulivu huku baadhi ya wafanya biashara wakifungua na kuendelea na biashara zao.  Katika vitongoji vya Bweyogerere na Kireka kulikuwa na maofisa wa kijeshi na polisi ambao walionekana wakipiga doria na kulinda biashara za watu.  Hali ya usalama pia ilionekana ikiimarisha katika barabara ya Entebbe. Naibu mkuu wa polisi katika mji wa Kampala Luke Owoyesigire amesema hali imerudi kawaida na kuwataka wafanya biashara kuondoa hofu na kuendelea na biashara zao kama kawaida. Katika soko la Kisekka wanajeshi na maofisa wa polisi walionekana wakikagua kila gari linalopita na kukagua vitambulisho vya kila mwendesha gari.