China kuendelea kuhimiza kazi za kupunguza umaskini duniani
2020-11-20 19:53:45| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, kuondoa umaskini wa aina zote ni changamoto kubwa zaidi inayoikabili dunia nzima, pia ni matakwa ya lazima katika kutimiza maendeleo endelevu.

Amesema China itaendelea kuhimiza kazi za kupunguza umaskini duniani, kuimarisha maingiliano kuhusu uzoefu wa kupunguza umaskini na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kupunguza umaskini.

Bw. Zhao Lijian amesema, mwaka huu wa 2020 ni mwaka wa mwisho wa China kutimiza ujenzi wa jamii yenye maisha bora, pia ni mwaka muhimu wa kutimiza lengo la kutokomeza umaskini kote nchini. Mwaka huu China itatimiza lengo la kuondoa umaskini kwenye maeneo yote ya vijijini, na hivyo kutimiza lengo hilo miaka 10 kabla ya muda uliopangwa wa kuondokana na umaskini katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na kutoa mchango wa kihistoria katika kutokomeza umaskini na kutimiza amani na maendeleo katika dunia nzima.