SOKA: FIFA kuilipa Liverpool, sababu Gomez
2020-11-20 16:28:50| cri

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), linataka kuilipa Liverpool kiasi cha pauni milioni mbili kwa ajili ya malipo ya mshahara wa beki wao, Joe Gomez ambaye aliumia kwenye timu yake ya Taifa ya England ilipokuwa kwenye mazoezi na anaweza kukaa nje kwa muda mrefu. Beki huyo ambaye aliumia goti analipwa pauni 80,000 kwa wiki akiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha ndefu Anfield. Fedha hizo zitalipwa na FIFA kwa kuwa wachezaji wa England wapo kwenye mradi wa msaada wa shirikisho kubwa la soka duniani, lakini, wakiwa na bima ambazo zinasimamiwa na Shirikisho hilo.