China yapenda kushirikiana na Afrika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye sekta ya afya
2020-11-20 19:55:32| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC katika kutekeleza matokeo yaliyofikiwa katika mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na mkutano maalumu wa kupambana na virusi vya Corona kati ya China na Afrika, kuimarisha ujenzi wa mfumo na uwezo wa kinga na udhibiti wa afya ya umma katika nchi za Afrika, kuinua uwezo wa nchi hizo wa kukabiliana na changamoto za magonjwa ya kuambikiza, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye sekta ya afya kati ya China na Afrika.

Bw. Zhao Lijian pia ameipongeza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na watu wake kutokana na kumalizika kwa mlipuko mpya wa Ebola nchini humo.