China yatoa wito kwa APEC iunge mkono mfumo wa kibiashara wa pande nyingi
2020-11-21 21:28:53| CRI

China yatoa wito kwa APEC iunge mkono mfumo wa kibiashara wa pande nyingi

Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) na kutoa hotuba kwa njia ya video.

Rais Xi alitoa wito kwa nchi na sehemu katika eneo la Asia na Pasifiki liunge mkono mfumo wa kibiashara wa pande nyingi ambao kiini chake ni Shirika la biashara duniani (WTO). Alisema China ina matumaini kuwa eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki litaanzishwa haraka iwezekanavyo.

Rais Xi aliongeza kuwa, kazi muhimu ya kwanza kwa hivi sasa ni kukabiliana na maambukizi ya janga la COVID-19, na China inaunga mkono jumuiya ya APEC iimarishe ushirikiano katika sekta za chanjo, afya ya umma na kampuni ndogo na za ukubwa wa katikati, ili kuchangia mapambano dhidi ya virusi vya Corona na juhudi za kufufua uchumi.