NDONDI: Francis Miyeyusho amtwanga kwa TKO mpinzani wake Deo Samweli
2020-11-23 16:47:52| cri

Bondia Francis Miyeyusho juzi alimtwanga kwa TKO, mpinzani wake, Deo Samweli katika pambano la raundi 8, lililopigwa Uwanja wa Kinesi uliopo Ubungo Shekilango Jijini Dar. Katika pambano hilo mabondia hao walioneshana upinzani mkali mpaka raundi ya mwisho kila mmoja akimuonesha mwenzake ubabe wa kivita. Raundi ya mpambano huo ikielekea ukingoni Miyeyusho aliitumia kipindi hicho kukusanya nguvu na kumshambulia mpinzani wake kwa ngumi nyingi mfululizo akiwa amembana kwenye kamba mpaka alipookolewa na mwamuzi wa mpambano huo, Pembe Ndava. Kwa kipigo hicho Miyeyusho alipata ushindi wa TKO dhidi ya mpinzani wake huyo.