Mkutano wa Internet Duniani wafunguliwa Wuzhen mkoani Zhejiang, China
2020-11-23 19:35:53| CRI

Mkutano wa Internet Duniani wafunguliwa Wuzhen mkoani Zhejiang, China

Mkutano wa Internet Duniani na Jukwaa la Maendeleo ya Internet umefunguliwa leo mjini Wuzhen mkoani Zhejiang mashariki mwa China, ambao umefuatilia uwezeshaji wa kidijitali na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja katika mambo ya mtandao.

Mkutano huo utajadili mada kuhusu kinga na udhibiti wa virusi vya Corona kisayansi, kuhimiza uchumi wa kidijitali na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na kusaidia kufufua uzalishaji mali.

Mkutano huo pia unatarajiwa kutoa ripoti ya mwaka 2020 kuhusu maendeleo ya mtandao wa Internet nchini China, na ripoti ya mwaka 2020 kuhusu mtandao wa Internet wa dunia.

Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwenye mkutano huo. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, kutumia fursa ya kihistoria ya mapinduzi ya kitaarifa (Information Revolution), kukuza msukumo mpya wa maendeleo yenye uvumbuzi, kuanzisha hali mpya ya ushirikiano wa kidijitali, kujenga muundo mpya wa usalama mtandaoni, kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kwenye mtandao wa Internet, na kushirikiana katika kujenga mustakabali mzuri zaidi wa binadamu.