UGANDA: WAUZA VILEO NA WASHIKA DAU KATIKA SEKTA HIYO WALALAMIKA HASARA KUBWA
2020-11-23 18:10:06| cri

Wasambazaji wa vileo na bidhaa zingine zinazohusiana na vileo wanasema kwamba wamepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 550 kwa miezi minane iliyopita, tangu serikali ilipotoa agaizo la baa na maeneo yote ya burudani kufungwa mnamo mmwezi Machi mwaka huu.

Wakizungumza na waandishi wa habarai jijini Kampla, waakilishi wa washika dau katika sekta hiyo wanasema kwamba wanaelewa fika athari za janga la corona, ila wanaomba kwamba waruhusiwe kurejelea kazi zao kwa masharti. Wanasema kwamba kufungwa kwa kazi zao hakujawaathiri wao tu, ila pia uchumi wa taifa zima kwa jumla. Serikali ya kitaifa imelegeza masharti makali kwa baadhi ya sekta za uchumi Uganda,isipokuwa setka ya uuzaji vileo na maeneo ya burudani.