TANZIA: Anele Ngcongca afariki dunia kwa ajali ya gari nchini Afrika Kusini
2020-11-24 16:54:37| cri

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, KRC Genk na Mamelodi Sundowns Anele Ngcongca, 33, amefariki dunia jana kwa ajali ya gari huko KwaZulu-Natal, nchini Afrika Kusini. Taarifa zinaeleza kuwa Anele amepata ajali akiwa katika BMW ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke ambaye yupo mahututi. Anele Ngcongca aliichezea timu ya Mamelodi Sundowns kwa miaka minne (2016-2020) baada ya kudumu na KRC Genk ya Ubelgiji kwa miaka tisa (2007-16). Beki huyo wa kulia hivi karibuni aliachana na mabingwa wa ligi kuu ya nchini  Afrika Kusini (PSL), Mamelodi Sundowns.