China yapenda kuchangia zaidi kwenye juhudi za binadamu za kuchunguza na kutumia anga za juu kwa njia ya amani
2020-11-24 19:06:16| CRI

China yapenda kuchangia zaidi kwenye juhudi za binadamu za kuchunguza na kutumia anga za juu kwa njia ya amani

Tarehe 24 alfajiri, China imerusha kwa mafanikio chombo cha uchunguzi kwenye mwezi cha Chang’e-5 kwa kutumia roketi ya Long March-5, na kuzindua safari ya kwanza ya China ya kukusanya na kurudisha sampuli kutoka kwenye Mwezi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China inapenda kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye juhudi za binadamu za kuchunguza na kutumia anga za juu kwa njia ya amani.  

Amesema, uchunguzi wa binadamu kwa ulimwengu hautasitishwa, na kuchunguza na kutumia anga za juu kwa amani ni mambo ya pamoja ya binadamu wote, ambayo yanapaswa kuhudumia maslahi ya binadamu wote. Amesema China siku zote inajitahidi kuchunguza na kutumia anga za juu kwa njia ya amani, na inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye juhudi za binadamu za kuchunguza na kutumia anga za juu kwa amani na pia kwenye ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.