Tanzania-ATCL kupokea ndege mpya mwezi ujao
2020-11-25 17:02:17| cri

Kampuni ya ndege ya Tanzania,ATCL inatarajia kupokea ndege mpya aina ya Bombadier Dash 8 Q400 mwishoni mwa mwezi ujao.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya ndege ya ATCL , Josephat Kagirwa jana alisema kuwa ingawa hawajapata tarehe rasmi ya kuwasili kwake ,lakini haitazidi mwisho wa mwezi ujao.

Aidha alidokeza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 78.

Hadi sasa serikali ya awamu ya tano Tanzania imenunua ndege mpya 11,8 zimeshawasili,moja ni hiyo inayotarajiwa Desemba na mbili zinaendelea kutengezwa.

Kagirwa alisema ndege mbili zilizobaki ambazo ni aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zitawasili nchini Tanzania mwakani.