Wakimbizi elfu 40 wa Ethiopia wakimbilia Sudan
2020-11-25 18:39:57| cri

Mpaka juzi, wakimbizi 41,193 kutoka Ethiopia wamekimbia machafuko katika jimbo la Tigray na kuingia nchi jirani ya Sudan.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa imesema, wakimbizi wanaishi katika mazingira magumu kwenye eneo la mpakani kati ya Ethiopia na Sudan, na shirika hilo linaendelea kuwapatia msaada.

Wakimbizi elfu 40 wa Ethiopia wakimbilia Sudan

Habari zinasema, tarehe 14, mwezi huu, wafuasi wa chama cha TPLF cha Tigray wameshambulia kambi ya jeshi la ulinzi la jimbo hilo na kujaribu kunyang’anya silaha zao nzito. Jimbo hilo limetangaza hali ya dharura kwa miezi sita.

Wakimbizi elfu 40 wa Ethiopia wakimbilia Sudan

Wakimbizi elfu 40 wa Ethiopia wakimbilia Sudan

Wakimbizi elfu 40 wa Ethiopia wakimbilia Sudan